Napenda kukukaribisha katika mkutano wa kwanza wa TAiN hapa Arusha Tanzania,TAiN ni kifupi cha maneno ya kiingereza yaitwayo Tanzania Adventist internet Network, maneno haya kwa tafsiri pana na yenye maana sahihi ni Mtandao wa Intaneti wa Waadventista Tanzania.
Wazo la kuanzia TAiN lilianzishwa mwaka 2014 na Watanzania watano ambao ni Mch. Steven Bina, Mch. Musa Mika, Mch. Aston Mmamba, Mch. Christopher Ungani na Ndg. Gideon Msambwa, waliohudhuria mkutano mkubwa ya idara ya mawasiliano duniani ufahamikao kama GAiN jijini Baltmore nchini Marekani. Walifurahishwa na majadiliano ya mkutano ule wa GAiN na wakapendekeza kuanzisha mikutano ya namna ile katika nchi yetu ya Tanzania. Ndipo likazaliwa jina la TAiN.
Lengo kuu la mkutano huu wa TAiN ni kujadili ubunifu na njia za kisasa za teknolojia ya mtandao ili kutimiza utume wa kanisa la Waadventista wa Sabato.
Mikutano ya namna hii itaendelea kufanyika kila mwaka, Mwaka 2016 mkutano wa TAiN utafanyika Dodoma.
Ni matumaini yangu kwamba utaondoka katika mkutano huu wa TAiN ukiwa umejazwa mawazo mapya na roho mtakatifu atakuongoza kutumia njia za kisasa za teknolojia ya mtandao kumtumikia Mungu katika eneo lako la kazi.
Tuungane pamoja tuuambie ulimwengu Yesu anakuja tena
Gideon T. Msambwa
Mratibu wa TAiN 2015